Swali: Ukhy kutoka Riyaadh anasema, yeye kaolewa sasa miaka kumi na hana watoto. Mume wake hahifadhi swalah zake. Yaani anaswali siku moja au mbili kisha anaacha kabisa. Nifanye kitu gani? Nihusieni, je, nitengane naye au hapana?

Jibu: Ikiwa anaacha swalah kabisa moja kwa moja. Haswali si Jamaa’ah, wala haswali peke yake, wala haswali kwa wakati wake, wala haswali nje ya wakati; basi itakuwa haijuzu wewe kubaki [kuishi] naye. Kwa kuwa mtu kama huyo atakuwa ni kafiri. Na wewe [mke] ni muislamu.

Na Allaah (Ta´ala) amesema:

“Mkiwa mnawajua kuwa ni waumini basi msiwarudishe [wanawake] kwa makafiri. Wanawake hao si halali kwa hao makafiri, basi wala hao makafiri hawahalalikii wanawake waumini.” (al-Mumtahinah 60 : 10)

Na ukafiri hapa kwa mujibu wa Hadiyth Swahiyh. Anasema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):

“Baina ya mja na ukafiri ni mtu kuacha swalah.”

Na katika Hadiyth nyingine:

“Ahadi iliyopo kati yetu na kati yao [makafiri] ni swalah, hivyo basi yule mwenye kuiacha amekufuru.”

Dalili zipo nyingi. Ikiwa ameacha swalah kabisa moja kwa moja, basi atakuwa siyo muislamu. Ila ikiwa atatubu kwa Allaah, na akawa mwenye kuhifadhi swalah. Ni lazima kwako mwanamke kumlingania. [Ikishindikana] mpeleke mahakama ya Kiislamu ya hakimu atalihukumu suala hilo.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://www.youtube.com/watch?v=ByZgJCeoG2o
  • Imechapishwa: 10/04/2022