Nimzuie mtoto wa miaka saba anapenda kwenda msikitini?

Swali 02: Kuna mtoto wa kiume ana miaka saba ambaye anafahamu na wala haudhi na anapenda kwenda msikitini. Je, akatazwe?

Jibu: Ikiwa haudhi hakuna neno. Kwa sababu kinachozingatiwa ni akili. Miaka saba ndio wakati wa kupata akili mara nyingi. Japokuwa wako wanaopata akili katika miaka saba na wengine baada ya hapo. Muhimu mtoto awe na akili na asiwaudhi watu.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 32
  • Imechapishwa: 25/07/2018