Ni ipi hukumu ya wudhuu´ wa aliyenuia kulala kisha asilale?

Swali 01: Kuna mtu amenuia kukata wuduu´ wake kwa kulala halafu hakulala tena. Je, atawadhe tena?

Jibu: Kulala hakufungamani na nia. Kumefungamana na hadathi. Iwapo atanuia kulala kisha asilale basi bado yuko juu ya twahara yake na wudhuu´ wake hauchenguki. Twahara yake haigeuki mpaka alale.  Hali kadhalika iwapo atanuia kupata hadathi kisha asipate hadathi wudhuu´ wake hauchenguki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 32
  • Imechapishwa: 25/07/2018