Swali: Je, kila anayekujia kukuomba unampatia?

Jibu:

وَفِي أَمْوَالِهِمْ حَقٌّ لِّلسَّائِلِ وَالْمَحْرُومِ

“Katika mali zao kuna haki maalum; kwa mwenye kuomba na asiyeomba.”[1]

Isipokuwa ikiwa utajua kwamba yeye ni muongo, basi mkemee na umnasihi. Ikiwa utamjua kuwa ni muongo, anastahili kuonywa na kufundishwa. Lakini ikiwa humjui au unajua kuwa ana haja ya kweli, basi Sunnah ni kumpa kadiri utakavyoweza.

[1] 51:19

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31164/هل-يعطى-كل-من-يسال
  • Imechapishwa: 09/10/2025