Nimfanye nini mnyama niliyemwokota?

Swali: Nimeokota kondoo wawili waliopotea. Nimeulizia kuhusu wamiliki katika maeneo mbalimbali na katika soko la mifugo, lakini sikuwapata. Naomba nipe fatwa nini nifanye nao?

Jibu: Mtu akiokota kondoo au mnyama mwingine kama ng’ombe na mfano wake katika wanyama wanaoweza kupotea au kuangamia, basi inampasa atangaze khabari zake kwa muda wa mwaka mzima. Akitambulika mmiliki, basi ni jambo jema, na asipotambulika anakuwa halali kwake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Atakayehifadhi mnyama aliyepotea bila kutangaza, basi yeye pia ni mwenye kupotea mpaka atangaze.”

Ama ng’ombe na ngamia, hawa wanaweza kujilinda wenyewe. Kwa hivyo hapaswi kuwachukua na kuwamiliki, bali waachwe jangwani mpaka wapatikane na wamiliki wao. Kama wako sokoni, basi wamiliki wao watawapata. Lakini kondoo na mbuzi anapaswa kutangazwa kwa mwaka mzima. Vivyo hivyo kwa wanyama wadogo wa kundi la kondoo na mbuzi ambao wanaweza kufa au kupotea kirahisi, hawa pia hutangazwa.

Hitimisho ni kwamba atangaze kwa mwaka mzima. Wakipatikana wamiliki wao ni vizuri, na wakikosekana wanakuwa halali kwake. Gharama za matangazo kwa mujibu wa maoni sahihi ni juu yake na anaweza kuzitoa kutoka katika mali aliyoipata. Akiacha na kutoichukua mali hiyo, hakuna tatizo.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1066/ما-يفعل-من-وجد-ضالة-الغنم
  • Imechapishwa: 21/01/2026