Swali: Baba yangu amefariki kwenda kwenye rehema za Allaah na amemuacha mama yangu ambaye ni mkubwa wa kiumri na ana watoto walio Riyaadh na nje yake. Sasa yuko ndani ya eda yake na anataka kuwatembelea au kuwatembelea wengine. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Mwanamke aliye ndani ya eda kwa sababu ya kufiwa na mume wake ni lazima akae nyumbani kwake. Asitoke, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kaa katika nyumba yako mpaka muda wa Kitabu ufike.”
Huyu anayekaa eda ni lazima akae nyumbani na asivae mavazi ya kupendeza, asitumie manukato, asipake wanja na wala asivae mapambo. Mambo matano ndani ya eda hayafai. Mnapaswa myahifadhi mambo haya matano:
1 – Kukaa nyumbani mpaka eda imalizike.
2 – Kutojivika nguo za kupendeza. Lakini avae nguo zisizo za kupendeza, ni mamoja iwe nyeusi, nyekundu, kijani au ya buluu muda wa kuwa sio ya mapambo.
3 – Kutojivika mapambo ya dhahabu, fedha, almasi, lulu na mengineyo. Asivae vito, wala saa ya mapambo, kwa kuwa hayo ni uzuri na pambo. Kwa hiyo yabaki mfukoni au sehemu nyingine.
4 – Kutojipaka wanja wala kuweka usoni pambo lolote wanalotumia wanawake leo isipokuwa maji na sabuni.
5 – Kuacha manukato.
Haya yote matano: kuacha manukato, kuacha mapambo, kuacha nguo nzuri… Lakini ikiwa kuna haja, kama daktari, dharurah ikamlazimisha kutoka kwenda kwa daktari kutafuta dawa, basi hakuna ubaya. Au kama hana wa kumhudumia, anatoka kwenda sokoni kwa haja zake, kama chakula au mboga, ikiwa hakuna anayemfanyia haja zake, hakuna ubaya kutoka. Lakini kutoka kwa ajili ya kuwatembelea watoto, basi hatoki kwa sababu hiyo.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1053/حكم-خروج-المراة-في-عدتها-لزيارة-اولادها
- Imechapishwa: 21/01/2026
Swali: Baba yangu amefariki kwenda kwenye rehema za Allaah na amemuacha mama yangu ambaye ni mkubwa wa kiumri na ana watoto walio Riyaadh na nje yake. Sasa yuko ndani ya eda yake na anataka kuwatembelea au kuwatembelea wengine. Ni ipi hukumu ya hilo?
Jibu: Mwanamke aliye ndani ya eda kwa sababu ya kufiwa na mume wake ni lazima akae nyumbani kwake. Asitoke, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Kaa katika nyumba yako mpaka muda wa Kitabu ufike.”
Huyu anayekaa eda ni lazima akae nyumbani na asivae mavazi ya kupendeza, asitumie manukato, asipake wanja na wala asivae mapambo. Mambo matano ndani ya eda hayafai. Mnapaswa myahifadhi mambo haya matano:
1 – Kukaa nyumbani mpaka eda imalizike.
2 – Kutojivika nguo za kupendeza. Lakini avae nguo zisizo za kupendeza, ni mamoja iwe nyeusi, nyekundu, kijani au ya buluu muda wa kuwa sio ya mapambo.
3 – Kutojivika mapambo ya dhahabu, fedha, almasi, lulu na mengineyo. Asivae vito, wala saa ya mapambo, kwa kuwa hayo ni uzuri na pambo. Kwa hiyo yabaki mfukoni au sehemu nyingine.
4 – Kutojipaka wanja wala kuweka usoni pambo lolote wanalotumia wanawake leo isipokuwa maji na sabuni.
5 – Kuacha manukato.
Haya yote matano: kuacha manukato, kuacha mapambo, kuacha nguo nzuri… Lakini ikiwa kuna haja, kama daktari, dharurah ikamlazimisha kutoka kwenda kwa daktari kutafuta dawa, basi hakuna ubaya. Au kama hana wa kumhudumia, anatoka kwenda sokoni kwa haja zake, kama chakula au mboga, ikiwa hakuna anayemfanyia haja zake, hakuna ubaya kutoka. Lakini kutoka kwa ajili ya kuwatembelea watoto, basi hatoki kwa sababu hiyo.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1053/حكم-خروج-المراة-في-عدتها-لزيارة-اولادها
Imechapishwa: 21/01/2026
https://firqatunnajia.com/mambo-matano-yasiyofaa-kwa-mwanamke-ndani-ya-eda/