Swali: Mara nyingi  natia shaka kama nimesujudu mara moja au mara mbili. Nifanye nini?

Jibu: Ikiwa ni wasiwasi, achana nao na utendee kazi vile inavyopelekea dhana yako kubwa. Lakini ikiwa ni kitu kinatokea mara fulani na haihusiani na wasiwasi, basi azingatie kile alichotia shaka hakipo, badala yake alete sijda nyingine na amalizie kwa sujuud ya kusahau.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (40)
  • Imechapishwa: 25/05/2023