Nimeomba kinga lakini bado nahisi wasiwasi?

Swali: Ni kwa nini kuna ambao wanaomba kinga kutokamana na shaytwaan kabla ya kuanza kusoma Qur-aan lakini pamoja na hivyo wanahisi kuwa shaytwaan anawashawishi na kuwatia wasiwasi?

Jibu: Kwa sababu ameomba kinga kwa ulimi wake tu na hakuhudhurisha maana ya uombaji kinga kwa moyo wake. Chenye kuzingatiwa sio matamshi peke yake. Kinachozingatiwa ni kuuhudhurisha moyo wakati wa kuomba kinga, mtu atambue maana ya kuomba kinga na aiamini ili aweze kunufaika na uombaji kinga huu.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Furqaan (01) http://alfawzan.af.org.sa/node/2044
  • Imechapishwa: 07/10/2016