Swali: Baadhi wanasema hii leo ni jambo la dharurah kuingia katika vyama kwa sababu ya kutengwa na vyama vingine. Unasemaje juu ya hilo?

Jibu: Hii sio dharurah. Hayo ni mawazo tu. Nyinyi mnafikiria kuwa ni dharurah. Lakini sio dharurah kabisa. Allaah (Jalla wa ´Alaa) amesema:

وَمَا جَعَلَ عَلَيْكُمْ فِي الدِّينِ مِنْ حَرَجٍ

“Hakukufanyieni ugumu wowote ule katika dini.”[1]

Je, vyamavyama hivi ni katika dini? Je, kuwagawanya waislamu ni katika dini? Vyama sio dharurah kabisa. Msifikiri kuwa mtapata mapenzi pale ambapo mtajiunga na chama fulani. Msifikiri mtapata haki zenu pale ambapo mtajiunga na chama fulani. Haya ni mawazo tu na uwongo. Sisi tunakufuru vyama na mapote yote isipokuwa tu chama na kipote kimoja: kundi la Allaah. Lakini hatusemi kuwa sisi pekee ndio kundi la Allaah na mapote mengine yote ni mapote ya shaytwaan. Bali tunasema kundi la Allaah lipo Yemen, Misri na Sudan, kati ya waarabu na wasiokuwa waarabu. Yako katika miji yote ya Kiislamu na linafanya kazi kwa ajili ya Allaah (´Azza wa Jall); wanalingania katika Qur-aan na Sunnah.

Ama wafuasi wa vyama ni wenye kubana, kwa sababu wanafupisha chama chao juu ya watu fulani. Kilicho cha wajibu ni kulingania ummah mzima wa Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Bali mtu akiweza kuwalingania makafiri katika Uislamu na unyoofu – bali akiweza hata kuwalingania majini afanye hivo. Lakini hawa waliobadilishwa huenda hata wakapanda juu ya milima na kuvua sauti. Mabedui ni wenye akili zaidi kuliko wao. Siku moja nilimuuliza bedui mmoja yuko katika chama gani. Bedui yule akasema kuwa yuko katika chama cha kibedui na anavicheka vyama vyote. Watu hawa wameathiriwa na maadui wa Uislamu na kwa kuwafuata kichwa mchunga…

Watu wa leo hawajali utapeli. Wanaweza hata kuwalaghai watu wa kawaida ilimradi tu kuwaingiza ndani ya vyama vyao. Wakomunisti wanaweza kuwaahidi watu kuwapa nyumba, kukuozesha msichana wake na kukupa magari ili tu uwape kura zao. Walakini, anayedanganywa huyu hajui kuwa wako tayari hata kuchukua nyumba, mke na gari yake.

Ahadi na uwongo. Hawaoni aibu kusema uwongo. Mambo ya vyamavyama vyote yamejengeka juu ya udanganyifu na uwongo. Chama fulani kilinitumia barua kuniomba maoni yangu. Sentensi mbili au tatu zilihusu Uislamu, zilizobaki ni ukafiri mtupu. Ukisoma vitabu vyao, unakuta uchupaji wa mipaka mtupu (الطَّاغُوتية).

[1] 22:78

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 359-361
  • Imechapishwa: 30/06/2025