Jiepushe na mihadhara inayochukuliwa video

Swali: Ni ipi hukumu ya zile video zinazoitwa za Kiislamu? Mtu afanye nini akiwa katika kikao ambapo kuna filamu hiyo?

Jibu: Ni picha. Abul-Hayyaaj ameeleza kwamba ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) alimwambia:

“Hivi nisikutume juu ya kazi aliyonituma kwayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Usiache picha hata moja isipokuwa umeiharibu wala kaburi lililoinuka isipokuwa umelisawazisha.”[1]

Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikataa kuingia chumba cha ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa) kilichokuwa na picha. Ni wajibu kwa muislamu kuzikemea akiweza au ajitenge mbali na vikao hvio:

“Ambaye ataona maovu katika nyinyi ayaondoshe kwa mkono wake, asipoweza afanye hivo kwa ulimi wake, asipoweza afanye hivo kwa moyo wake – na hiyo ni imani dhaifu kabisa.”[2]

Watu hawa si jengine isipokuwa tu ni wafuata kichwa mchunga. Yule ambaye anasimama juu ya mimbari na watu wanamchukua video ni mwenye kukubali maovu. Mtu hastahiki kuhudhuria kikao chake. Bali waislamu wanapaswa kujitenga mbali na vikao vyake. Allaah awajaze kheri vijana wa Riyaadh waliovunja camera iliowekwa mbele ili kurekodi muhadhara. Ima uvunja camera hiyo au uikaripie kwa mdono wako. Usipoweza chochote katika hayo mawili basi nakushauri kujitenga na muhadhara huu uliochafuliwa na madhambi.

[1] Muslim (969).

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 376
  • Imechapishwa: 30/06/2025