Swali 6: Ni zipi adabu za safari kwa ajili ya Hajj?
Jibu: Adabu za safari ya Hajj zinagawanyika katika sehemu mbili:
1 – Adabu za lazima.
2 – Adabu zinazopendekezwa.
Adabu za lazima ni kwamba afanye mtu yale mambo ya wajibu ya Hajj na nguzo zake, ajiepushe na yaliyokatazwa ya Ihraam maalum na yaliyokatazwa ya jumla, yaliyokatazwa katika Ihraam na katika hali isiyo ya Ihraam. Allaah (Ta´ala) amesema:
الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ
“Hajj [inatakiwa kutekelezwa katika] miezi maalum. Yule ambaye imemfaradhikia [katika miezi hiyo kwa kupata uwezo wa kwenda] hajj basi asifanye jimaa, ufasiki wala mabishano.”[1]
Kuhusu adabu zinazopendekezwa katika safari ya Hajj ni kwamba afanye mtu kila ambalo inapasa kwake kulifanya, katika ukarimu wa nafsi, mali, hadhi, kuwatumikia ndugu zake, kuvumilia maudhi yao, kujizuia na maovu yao na kuwafanyia wema. Ni mamoja hilo liwe baada ya kuingia ndani ya Ihraam au kabla ya kuingia kwake katika Ihraam, kwa sababu hizi adabu ni za juu zenye ubora ambazo zinatakiwa kutoka kwa kila muumini katika kila wakati na mahali. Vilevile adabu zinazopendekezwa katika nafsi ya kufanya ´ibaadah, kama vile kwamba mtu afanye Hajj kwa namna iliyo kamili zaidi na hivyo anajitahidi kuikamilisha kwa adabu za maneno na matendo, ambazo huenda tukapata nafasi ya kizizungumzia katika maswali mengine.
[1] 02:197
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/16-17)
- Imechapishwa: 01/06/2026
Swali 6: Ni zipi adabu za safari kwa ajili ya Hajj?
Jibu: Adabu za safari ya Hajj zinagawanyika katika sehemu mbili:
1 – Adabu za lazima.
2 – Adabu zinazopendekezwa.
Adabu za lazima ni kwamba afanye mtu yale mambo ya wajibu ya Hajj na nguzo zake, ajiepushe na yaliyokatazwa ya Ihraam maalum na yaliyokatazwa ya jumla, yaliyokatazwa katika Ihraam na katika hali isiyo ya Ihraam. Allaah (Ta´ala) amesema:
الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ
“Hajj [inatakiwa kutekelezwa katika] miezi maalum. Yule ambaye imemfaradhikia [katika miezi hiyo kwa kupata uwezo wa kwenda] hajj basi asifanye jimaa, ufasiki wala mabishano.”[1]
Kuhusu adabu zinazopendekezwa katika safari ya Hajj ni kwamba afanye mtu kila ambalo inapasa kwake kulifanya, katika ukarimu wa nafsi, mali, hadhi, kuwatumikia ndugu zake, kuvumilia maudhi yao, kujizuia na maovu yao na kuwafanyia wema. Ni mamoja hilo liwe baada ya kuingia ndani ya Ihraam au kabla ya kuingia kwake katika Ihraam, kwa sababu hizi adabu ni za juu zenye ubora ambazo zinatakiwa kutoka kwa kila muumini katika kila wakati na mahali. Vilevile adabu zinazopendekezwa katika nafsi ya kufanya ´ibaadah, kama vile kwamba mtu afanye Hajj kwa namna iliyo kamili zaidi na hivyo anajitahidi kuikamilisha kwa adabu za maneno na matendo, ambazo huenda tukapata nafasi ya kizizungumzia katika maswali mengine.
[1] 02:197
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/16-17)
Imechapishwa: 01/06/2026
https://firqatunnajia.com/ni-zipi-adabu-za-safari-kwa-ajili-ya-hajj/