Swali 12: Nini maana ya maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ
”Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.”[1]?
Jibu: Allaah (Ta´ala) ametumia maneno:

”Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.”
kwa sababu hakushikamana na nguzo za Uislamu. Kufuru hutumika kwa yale yaliyo chini ya shirki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mambo mawili katika watu ni kufuru: kutia dosari katika nasaba na kumuombolezea maiti.”[2]
Kuna maafikiano kwamba mtu hatoki katika dini kwa ajili ya mambo hayo. Kilichotufanya kutia nguvu maoni haya ni kwamba ´Abdullaah bin Shaqiyq (Rahimahu Allaah) – naye ni miongoni mwa wanafunzi wakubwa wa Maswahabah wanaotambulika – amesema:
“Hakuna kitu katika matendo Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiona kukiacha ni ukafiri isipokuwa swalah.”[3]
[1] 03:97
[2] Muslim (67).
[3] at-Tirmidhiy (2622).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/23)
- Imechapishwa: 01/06/2026
Swali 12: Nini maana ya maneno Yake Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala):
وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ
”Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.”[1]?
Jibu: Allaah (Ta´ala) ametumia maneno:
وَمَن كَفَرَ فَإِنَّ اللَّـهَ غَنِيٌّ عَنِ الْعَالَمِينَ
”Na atakayekanusha, basi hakika Allaah ni mkwasi kwa walimwengu.”
kwa sababu hakushikamana na nguzo za Uislamu. Kufuru hutumika kwa yale yaliyo chini ya shirki. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
”Mambo mawili katika watu ni kufuru: kutia dosari katika nasaba na kumuombolezea maiti.”[2]
Kuna maafikiano kwamba mtu hatoki katika dini kwa ajili ya mambo hayo. Kilichotufanya kutia nguvu maoni haya ni kwamba ´Abdullaah bin Shaqiyq (Rahimahu Allaah) – naye ni miongoni mwa wanafunzi wakubwa wa Maswahabah wanaotambulika – amesema:
“Hakuna kitu katika matendo Maswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) walikuwa wakiona kukiacha ni ukafiri isipokuwa swalah.”[3]
[1] 03:97
[2] Muslim (67).
[3] at-Tirmidhiy (2622).
Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/23)
Imechapishwa: 01/06/2026
https://firqatunnajia.com/maana-ya-kukufuru-ibaadah-ya-hajj/