Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Nguzo ya pili ni kuleta Takbiyr ya kufungulia swalah. Dalili ni Hadiyth inayosema:
“Uharamu [ufunguzi] wake ni Takbiyr na uhalali [ufungwaji] wake ni Tasliym.”[1]
Baada ya hilo kunakuja du´aa ya kufungulia, ambayo ni Sunnah, kwa kusema:
سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ وَبِحَمْدِكَ وتَبَارَكَ اسْمُكَ وَتَعَالى جَدُّكَ وَلا إِله غَيْرُكَ
“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah, kutokamana na kasoro zote na himdi zote ni Zako. Limetukuka jina Lako, ufalme Wako ni mkubwa na hapana mungu wa haki mwengine asiyekuwa Wewe.”[2]
Maana ya:
سُبْحَانَكَ اللَّهُمَّ
“Kutakasika ni Kwako, ee Allaah… ”
ni kwamba ninakutakasa kutokamana na kasoro zote kwa namna inayolingana na Utukufu Wako.
Maana ya:
وَبِحَمْدِكَ
“… na himdi zote ni Zako.”
ni kuwa Unahimidiwa.
Maana ya:
وتَبَارَكَ اسْمُكَ
“Limetukuka jina Lako… “
ni kuwa baraka hufikiwa kwa kutajwa Kwako.
Maana ya:
وَتَعَالى جَدُّكَ
”… ufalme Wako ni mkubwa.”
ni kuwa Utukufu Wako ni Mkubwa.
Maana ya:
وَلا إِله غَيْرُكَ
“Hapana mungu mwengine asiyekuwa Wewe.”
ni kwamba hakuna mwabudiwa wa haki katika ardhi wala mbinguni isipokuwa ni Wewe, Allaah.
MAELEZO
Kusoma du‘aa ya kufungua swalah kimyakimya baada ya Takbiyr ya kufungulia swalah na kabla ya kuanza kusoma ni katika Sunnah na mambo yanayopendekezwa katika swalah. Ni jambo limethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) kwa matamshi mbalimbali. Hivyo basi mwenye kuswali atachagua mojawapo katika swalah yake. Haifai kuzikusanya zote ndani ya swalah moja. Du‘aa iliyotajwa hapa na Shaykh ni mojawapo. Imesimuliwa na ‘Umar, ‘Aaishah na Abu Sa‘iyd (Radhiya Allaahu ‘anhum). Pia angalia ”Irwaa’-ul-Ghaliyl” (340) na (341).
Kisha Shaykh (Rahimahu Allaah) akasherehesha maana ya du‘aa hiyo, ambapo ndani yake kuna kumtakasa na kumsifu Allaah kwa namna inavyompasa Yeye. Maneno yake mtunzi (Rahimahu Allaah):
وتَبَارَكَ اسْمُكَ
“Limetukuka jina Lako… “
linatokana na neno baraka. Maana yake ni kuwa kila kheri na baraka hupatikana kwa kumtaja Allaah tu (Subhaanahu wa Ta´ala). Amesema (´Azza wa Jall):
أَلَا بِذِكْرِ اللَّـهِ تَطْمَئِنُّ الْقُلُوبُ
“Zindukeni! Kwa kumtaja Allaah nyoyo hutulia!”[3]
فَاذْكُرُونِي أَذْكُرْكُمْ
“Basi nidhukuruni na Mimi nitakukumbukeni!”[4]
Amesema (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam):
“Mfano wa yule anayemtaja Mola wake na yule asiyemtaja Mola wake ni mfano wa aliye hai na maiti.”
Ameipokea al-Bukhaariy (6407) kupitia kwa Abu Muusa (Radhiya Allaahu ‘anh).
Huenda vilevile maana ya “jina” ikawa na maana ya majina yote ya Allaah, kwa kuwa neno la umoja limetajwa kwa namna ya kutaja mengi, ni kama maneno Yake (Ta´ala):
وَإِن تَعُدُّوا نِعْمَةَ اللَّـهِ لَا تُحْصُوهَا
“Mkihesabu neema za Allaah hamtoweza kuzidhibiti.”[5]
Maneno yake mtunzi (Rahimahu Allaah):
وَتَعَالى جَدُّكَ
”… ufalme Wako ni mkubwa.”
Ni kama mfano wa maneno Yake:
وَأَنَّهُ تَعَالَىٰ جَدُّ رَبِّنَا مَا اتَّخَذَ صَاحِبَةً وَلَا وَلَدًا
“Na kwamba hakika umetukuka kabisa utukufu wa Mola wetu, hakujifanyia mke wala mwana.”[6]
Maneno haya matatu yaliyotajwa katika du´aa ”Subhaanaka”, ”Tabaaraka” na ”Ta´aalaa” hayatamkwi isipokuwa kwa ajili ya Allaah (Ta´ala). Haifai kusema kwa yeyote mwingine: “Umetasika na mapungufu”, “Umebarikika”, “Umetukuka” wala kuyakusanya yote matatu.
[1] Abu Daawuud (61), at-Tirmidhiy (3), Ibn Maajah (275) na Ahmad (01/123) kutoka katika Hadiyth ya ´Aliy bin Abiy Twaalib (Radhiya Allaahu ´anh). an-Nawawiy amesema:
”Hadiyth hii ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy na wengineo kwa cheni ya wapokezi Swahiyh. Isipokuwa tu ndani yake yuko ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Aqiyl.” (al-Majmuu´ (03/240)).
at-Tirmidhiy amesema:
”Hadiyth hii ndio Swahiyh zaidi juu ya maudhui haya au nzuri. ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Aqiyl ni mkweli. Baadhi ya wanachuoni wamemtia walakini kabla ya hifdhi yake. Abu ´Iysaa amesema: ”Ahmad bin Hanbal, Ishaaq bin Raahuuyah na al-Humaydiy walikuwa wakijengea hoja kwa Hadiyth ya ´Abdullaah bin Muhammad bin ´Aqiyl.” Ahmad amesema: ”Hadiyth zake ni njema.”
[2] Abu Daawuud (775), at-Tirmidhiy (243) na Ibn Maajah (806) kutoka katika Hadiyth ya ´Aiashah (Radhiya Allaahu ´anhaa).
at-Tirmidhiy:
”Hadiyth hii hatuijui kutoka katika Hadiyth ya ´Aaishah isipokuwa kwa wajhi hii. Haarithah ametiwa dosari kabla ya hifdhi yake.”
al-Haakim amesema:
”Hadiyth hii ni yenye cheni ya wapokezi Swahiyh na hakuitoa [al-Bukhaariy].” (al-Mustadrak (01/360)).
an-Nawawiy amesema:
”Ameipokea at-Tirmidhiy, Abu Daawuud na Ibn Maajah kwa cheni ya wapokezi dhaifu. Ameidhoofisha Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, al-Bayhaqiy na wengineo. Pia ameipokea Abu Daawuud, at-Tirmidhiy, an-Nasaa´iy, Ibn Maajah na al-Bayhaqiy kupitia kwenye upokezi wa Abu Sa´iyd al-Khudriy na ameidhoofisha.” (al-Adhkaar, uk. 360). Vilevile tazama “al-Majmuu´ (03/265).
[3] 13:28
[4] 2:152
[5] 16:18
[6] 72:03
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 45-46
- Imechapishwa: 01/06/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 45-46
Imechapishwa: 01/06/2026
https://firqatunnajia.com/39-nguzo-ya-pili-ya-swalah-ni-takbiyrat-ul-ihraam/