Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:
Nguzo za swalah ni kumi na nne:
1 – Kusimama kwa mwenye kuweza.
2 – Takbiyr ya kufungulia swalah.
3 – Kusoma al-Faatihah.
4 – Rukuu´.
5 – Kuinuka kutoka katika Rukuu´.
6 – Kusujudu juu ya viungo saba.
7 – Kuinuka kutoka katika Sujuud.
8 – Kukaa baina ya sujuud mbili.
9 – Utulivu katika nguzo zote.
10 – Kupangilia.
11 – Tashahhud ya mwisho.
12 – Kukaa katika Tashahhud ya mwisho.
13 – Kumswalia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).
14 – Tasliym.
MAELEZO
Nguzo ya kitu katika lugha ni upande wake wa nguvu zaidi.
Swalah katika lugha maana yake ni du´aa. Katika istilahi ya Shari´ah swalah ni maneno na matendo maalum yanayoanzishwa kwa Takbiry na kumalizika kwa salamu.
Nguzo za swalah ni sehemu ya ndani ya swalah. Tofauti kati ya sharti na nguzo ni kuwa nguzo ni sehemu ya swalah yenyewe iliyo ndani yake, wakati sharti si sehemu ya swalah, bali ni kitu kilicho kabla yake au kinachoambatana nayo, kama vile twahara au kuelekea Qiblah. Maneno yake mtunzi (Rahimahu Allaah):
”Nguzo ya kwanza ni kusimama kwa mwenye kuweza. Dalili ni Kauli Yake (Ta ´ala):
حَافِظُوا عَلَى الصَّلَوَاتِ وَالصَّلَاةِ الْوُسْطَىٰ وَقُومُوا لِلَّـهِ قَانِتِينَ
”Zichungeni swalah na khaswa khaswa swalah ya katikati na simameni mbele ya Allaah hali ya kuwa ni wanyenyekevu.”
Ni wajibu katika swalah ya faradhi kwa mtu kuiswali akiwa amesimama ikiwa anaweza.
Mtu anayeswali akiwa amekaa ilihali anaweza kusimama, basi swalah yake haisihi. Dalili ya hilo ni Hadiyth ya ‘Imraan bin Huswayn (Radhiya Allaahu ‘anh) ambaye ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) amesema:
“Swali kwa kusimama, usipoweza basi kwa kukaa, usipoweza basi kwa ubavu.”
Ameipokea al-Bukhaariy.
Lakini inafaa kuswali kwa kuketi chini katika swalah ya kujitolea, ingawa thawabu zake ni nusu ya thawabu ya anayeiswali akiwa amesimama. Kilicho bora zaidi ni kuiswali akiwa amesimama ili apate thawabu kamili. Hilo ni kutokana na Hadiyth ya ‘Abdullaah bin ‘Amr bin al-‘Aasw (Radhiya Allaahu ‘anhumaa) kuhusu jambo hilo. Ameipokea Msulim (735).
Iwapo mgonjwa hawezi kuswali akiwa amesimama ambapo akaswali swalah ya faradhi na ya kujitolea akiwa ameketi chini, basi atapata thawabu kamili. Hilo ni kutokana na maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa sallam) katika Hadiyth ya Abu Muusa (Radhiya Allaahu ‘anh):
“Mja anapougua au kusafiri huandikiwa mfano wa yale aliyokuwa akiyafanya akiwa mzima na mkazi.”
Ameipokea al-Bukhaariy (2996).
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 43-45
- Imechapishwa: 01/06/2026

Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 43-45
Imechapishwa: 01/06/2026
https://firqatunnajia.com/38-nguzo-ya-kwanza-ya-swalah-ni-kusimama/