Shaykh-ul-Islaam na Imaam Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (Rahimahu Allaah) amesema:

Sharti ya tisa ni nia na mahala pale ni moyoni. Kuitamka ni Bid´ah. Dalili ni Hadiyth:

“Matendo huzingatiwa kwa nia. Kila mmoja atalipwa kutokana na kile alichonuia.”[1]

MAELEZO

Nia katika swalah na ´ibaadah nyingine ni sharti. Kwa maana ya kwamba swalah haisihi bila ya nia. Amesema (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

“Hakika kila kitendo kinalipwa kutegemea na nia.”

Ameipokea al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).

Kwa nia hutofautishwa kati ya faradhi na faradhi nyingine, au kati ya faradhi na Sunnah. Tumetangulia wakati tulipokuwa tunazungumzia kwamba nia ni sharti miongoni mwa sharti za wudhuu´ ya kwamba haijuzu kwa mtu kutamka kwa ulimi wake yale aliyokusudia moyoni, isipokuwa katika ´ibaadah ya Hajj na ´Umrah ndio inajuzu kutamka yale aliyonuia kwa kusema:

لبيك عمرة

”Nimekuitikia ´Umrah.”

au:

لبيك حجّاً

”Nimekuitikia Hajj.”

au:

لبيك حجّاً وعمرة

”Nimekuitikia Hajj na ´Umrah.”

[1] al-Bukhaariy (1) na Muslim (1907).

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-Muhsin bin Hamad al-´Abbaad
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Shuruwt-is-Swalaah, uk. 42
  • Imechapishwa: 01/06/2026