Ni wenye kupata faida kwa hali yoyote

Swali: Kuna mtu alitokewa na ajali ya gari. Kwa vile alikuwa hakuilipia bima gari yake akatiwa jela kipindi fulani. Alipotoka nje akailipia gari bima yake na akasema kuwa hiyo ni dharurah. Je, hali hii ni dharurah?

Jibu: Kuna dharurah? Hakuna dharurah. Pindi mtu anapolipia bima gari yake na akatokewa na ajali  ambapo akapata fidia ya uharibifu kutoka katika bima, je, kampuni ya bima humlipa kile kima chote alichotoa? Je, kima kinachotolewa na shirika hili la bima kinalingana na kile kiwango chote cha pesa alicholipa ili kitendo hicho kiwe chenye kufaa? Lau mashirika ya bima yangelikuwa si yenye kujua kuwa yanapata faida basi yasingelikuwa ni yenye kufunguliwa kamwe.

  • Mhusika: ´Allaamah Swaalih bin Muhammad al-Luhaydaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://www.youtube.com/watch?v=CXNWVtd2O0U&feature=youtu.be
  • Imechapishwa: 16/01/2021