Ni wapi hutazama mswaliji anapokuwa katika Rukuu´, Sujuud na Tashahhud?

Swali: Mswaliji wakati wa kusimama kwake kunyooka sawasawa hutazama maeneo pa Sujuud yake. Ni wapi anatakiwa kutazama wakati wa Rukuu´, Sujuud na Tashahhud?

Jibu: Mswaliji katika hali ya Rukuu´ yake anatakiwa kutazama mahali pa Sujuud yake pia. Kuhusu wakati wa Tashahhud anatakiwa kutazama kidole chake cha kuashiria. Wakati wa Sujuud yake anatakiwa kutazama mbele kwa chini ya macho yake ardhini.

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

´Abdur-Razzaaq ´Afiyfiy

´Abdullaah bin Ghudayyaan

´Abdullaah bin Qu´uud

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (6914)
  • Imechapishwa: 22/05/2022