Swali: Nimesoma kwenye kitabu kuwa Salaf walikuwa wakitahadharisha wapiga visa. Ni kina nani wapiga visa? Je, inafaa kumhukumu mwenye kusimulia visa kwenye mawaidha ya kwamba ni mpiga visa na hivyo ni wajibu kuachana naye na kutosikiliza kanda zake?

Jibu: Mpiga visa ni yule anayewatolea watu mawaidha. Anaweza kutumia Hadiyth dhaifu na visa vya uongo ili tu aweze kuwaathiri watu pasina kujali usahihi wa Hadiyth au usahihi wa kisa. Yeye muhimu wake tu ni kutaka kuwaathiri watu. Hili halijuzu. Ni wajibu kwa mtu kama huyu kukemewa.

Kuhusiana na yule mwenye kusimulia visa ambavyo ni sahihi na vikawaathiri watu, hili ni jambo zuri. Allaah Amesimulia visa kwenye Qur-aan. Visa vya nyumati zilizotangulia, Manabii, watu wema n.k. Ametaja haya katika Qur-aan. Allaah (Ta´ala) amesema:

فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ

“Basi simulia visa huenda wakazingatia.” (06:176)

Ni sawa endapo kisa kitakuwa ni sahihi. Haijuzu kukitaja kisa pale ambapo kitakuwa ni dhaifu au hakina msingi.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: at-Tafsiyr al-Mufasswal (02)
  • Imechapishwa: 17/08/2020