Ni wajibu kuomba ulinzi dhidi ya mambo manne katika Tashahhud?

Swali: Kuomba ulinzi dhidi ya mambo manne haya ni jambo la wajibu au Sunnah?

Jibu: Kikosi cha wanazuoni wengi wanaona kuwa ni Sunnah. Imepokelewa kutoka kwa Twawuus ya kwamba alikuwa akimwamrisha mwanawe kuirudia swalah pale anapoiacha, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyaamrisha:

“Anapoleta Tashahhud mmoja wenu basi aombe kinga kwa Allaah dhidi ya mambo manne… “

Kwa hivyo muumini anatakiwa asiyaache ingawa wanazuoni wengi wanayaona kuwa ni Sunnah. Hata hivyo anatakiwa asiyaache, kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ameyaamrisha.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23780/هل-التعوذ-من-اربع-في-التشهد-واجب-ام-سنة
  • Imechapishwa: 27/04/2024