Ni wajibu kufanya walima kwa ajili ya kutangaza ndoa

Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Fanya walima ijapo kondoo mmoja.”[1]

Amri inafahamisha kuwa kufanya walima ni lazima?

Jibu: Inawezekana. Msingi wa amri ni ulazima. Kilichotangaa kwa wanazuoni ni kwamba inapendeza. Kufanya karamu ya ndoa ni Sunnah na ni kwa lengo la kutangaza ndoa. Aulizwe dalili. Pengine usahihi ni kwamba yeye (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alifanya walima pia wa isiyokuwa kondoo. Wakati alipomuoa Swafiyyah alifanya karamu ya ndoa kwa isiyokuwa nyama. Alifanya karamu ya ndoa ya uji, tende, maziwa ya maji na maziwa ya unga.

Swali: Nakusudia kwamba msingi wa walima ni lazima?

Jibu: Kwa minajili ya kutangaza ndoa. Udhahiri – na Allaah ndiye mjuzi zaidi – ni kwamba ni wajibu. Udhahiri wa maandiko ni uwajibu, kwa sababu hivo ni katika kutangaza ndoa. Ndoa inatangazwa kwa kufanya walima na kuwakusanya wale watu mtu atakaoweza.

[1] al-Bukhaariy (04/232), an-Nasaa´iy (02/93), Ibn Sa´d (03/02/77), all-Bayhaqiy (07/258), Ahmad (03/165) na wengineo.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23856/هل-تجب-الوليمة-في-اعلان-النكاح
  • Imechapishwa: 21/05/2024