Ni wajibu katika Tayammum kuanza kupangusa uso au inapendeza tu?

Swali: Kuanza kupangusa uso katika Tayammum ni lazima au inapendeza tu?

Jibu: Lazima:

فَامْسَحُوا بِوُجُوهِكُمْ وَأَيْدِيكُم مِّنْهُ

”… panguseni kwayo nyuso zenu na mikono yenu.”

“Anzeni kwa yale aliyoanza nayo Allaah.”

Kama alivosema Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akianza kwa uso.

Swali: Ambaye ametenganisha kati ya mwenye kufanya Tayammum kwa hadathi ndogo basi analazimika kuanza kupangusa uso, na mwenye kufanya Tayammum kwa hadathi ndogo inafaa kwake?

Jibu: Hapana. Uso ndio unaotangulizwa katika hali zote, kama anavofanya katika maji.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23576/هل-تقديم-الوجه-في-التيمم-واجب-ام-مستحب
  • Imechapishwa: 15/02/2024