Ni vipi mzazi atahakikisha uadilifu kati ya watoto?

Swali: Je, ni katika kufanya uadilifu kati ya watoto – wavulana na wasichana – kwa kuwanunulia yale wanayohitajia au kuwanunulia kunategemea na haja?

Jibu: Kuwanunulia yale wanayohitajia ndio maana ya kuwanunulia kutokana na haja. Maneno haya hayatofautiani. Ni lazima kufanya uadilifu kati ya watoto isipokuwa kwa kile anachokihitajia mmoja pasi na mwengine. Kwa mfano mtu ana watoto watatu ambapo mmoja katika wao amefikia umri wa kuoa. Katika hali hii anatakiwa kumuozesha na asiwape wale wengine kiasi alichompa. Kwa sababu hawajafikisha umri wa kuoa. Akiwa na msichana na mvulana ambapo mvulana anahitajia Riyaal ishirini ili anunue kilemba na msichana anahitajia mapambo ambapo ni pesa mia au mia mbili. Anatakiwa kumpa kila mmoja kile anachohitajia. Ama akitaka kuwapa kitu kilicho zaidi ya haja basi anatakiwa kusawazisha kati ya wavulana na wasichana ambapo mvulana awe na fungu la wasichana wawili.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (74) http://binothaimeen.net/content/1732
  • Imechapishwa: 27/08/2020