3174- Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haachi Rak´ah mbili kabla ya Fajr na Rak´ah mbili baada ya ´Aswr.
Ameipokea Ibn Abiy Shaybah katika ”al-Muswannaf” (2/352): ´Affaan ametuhadithia: Abu ´Awaanah ametuhadithia: Ibraahiym bin Muhammad bin al-Muntashir ametuhadithia, kutoka kwa baba yangu ambaye alikuwa akiswali Rak´ah mbili baada ya ´Aswr. Wakati alipoulizwa akasema:
”Nisingeziswali isipokuwa ni kwa sababu nilimuona Masruuq akiziswali, pamoja na kwamba alikuwa ni mtu mwaminifu. Lakini nikamuuliza ´Aaishah kuhusu jambo hilo ambapo akasema:
”Alikuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) haachi Rak´ah mbili kabla ya Fajr na Rak´ah mbili baada ya ´Aswr.”
Miongoni mwa makosa yaliyoenea katika vitabu vya Fiqh ni pale wanapokataza Rak´ah mbili hizi bali na kutozitaja miongoni mwa jumla ya Sunnah za Rawaatib, pamoja na kwamba zimethibiti kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akidumu kwazo kama ambavyo alikuwa akidumu kuswali Rak´ah mbili za kabla ya Fajr. Hakuna dalili yoyote inayoonyesha kuwa zimefutwa au kwamba ni mambo maalum kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) pekee. Ni vipi iwe hivyo ilihali mjuzi zaidi wa watu alikuwa akizihifadhi, naye si mwengine ni mama wa waumini ´Aaishah (Radhiya Allaahu ´anhaa), na Maswahabah na Salaf wengine walioafikiana naye?
Aidha inatakiwa kutambulika kwamba zile Hadiyth zilizokuja kwa jumla zinazokataza kuswali baada ya ´Aswr zimekuja kwa njia iliyofungamana kwa Hadiyth zengine Swahiyh ambazo zimesema wazi kwamba inafaa kuswali midhali jua bado halijakuwa manjano. Moja katika Hadiyth hizo ni ile ya ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) inayosema:
”Msiswali baada ya ´Aswr isipokuwa mkiswali jua liwe limeshainuka.”
Hadiyth ni Swahiyh na imepokelewa kwa njia nyingi.
- Muhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/1/528)
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)
Related
Swalah ya sunnah moja kwa moja baada ya ´Aswr
3173- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Umefanya vizuri Ibn-ul-Khattwaab.” Ameipokea Ahmad: Muhammad bin Ja´far ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa al-Azraq bin Qays, kutoka kwa ´Abdullaah bin Rabaah, kutoka kwa mmoja katika Mswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa…
In "Rawaatib na Nawaafil"
Sunnah ya Raatibah inamtosha mtu kutohitajia Tahiyyat-ul-Masjid
Swali: Je, Sunnah ya Raatibah inamtosheleza mtu kutohitajia Tahiyyat-ul-Masjid? Jibu: Sunan za Rawaatib zilizohifadhiwa katika Hadiyth Swahiyh kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) ni Rak´ah kumi na mbili; Rak´ah nne kabla ya Dhuhr kwa salamu mbili, Rak´ah mbili baada ya Dhuhr, Rak´ah mbili baada ya Maghrib, Rak´ah mbili…
In "Tahiyyat-ul-Masjid - Swalah ya mamkuzi ya msikiti"
Ndio maana ´Umar alikuwa akichapa
3173- Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema: “Umefanya vizuri Ibn-ul-Khattwaab.” Ameipokea Ahmad: Muhammad bin Ja´far ametuhadithia: Shu´bah ametuhadithia, kutoka kwa al-Azraq bin Qays, kutoka kwa ´Abdullaah bin Rabaah, kutoka kwa mmoja katika Mswahabah wa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam): “Baada ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa…
In "Rawaatib na Nawaafil"