Ni nani aliyekwambia tunasherehekea wiki Ibn ´Abdil-Wahhaab?

Swali: Baadhi ya wale wanaosherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) wanasema kuwa ni kwa nini inafaa kwenu kusherehekea wiki ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab na wala isifae kwetu kusherehekea mazazi ya Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)?

Jibu: Hatukushehekea wiki ya Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab. Ni nani aliyesema hivi? Kilichofanyika ni kuchapisha na kueneza vitabu vyake na pia kubainisha na kupambanuliwa ulingano wake (Rahimahu Allaah). Hiki ndicho kilichofanyika.

  • Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Majiyd (73)
  • Imechapishwa: 09/04/2025