Swali: Mtu ambaye si msomi afanye nini pale ambapo mwanachuoni mmoja anasema kuwa mtu fulani ni mzushi na mwengine akasema kuwa ni katika Ahl-us-Sunnah?  Ni sahihi kwamba itumike kanuni ya kujeruhi na kusifu?

Jibu: Kujeruhi na kusifu ni jambo linatendewa kazi na Muhaddithuun, na si wakina nyinyi. Kuwazungumzia watu na kuwagawanya kati ya wazuri na wabaya ni usengenyaji na uvumi. Sio kujeruhi na kusifu. Kujeruhi na kusifu inahusiana na elimu ya mlolongo wa wapokezi na hali za wapokezi. Inatakiwa kutendewa kazi na Muhaddithuun na sio na kila mtu.

Tabdiy´ inafanywa kwa mtu anayefanya Bid´ah au kuzusha. Yule mwenye kuzusha au kutendea kazi Bid´ah hata kama haikuizusha yeye ni mzushi:

“Mwenye kuzua katika dini yetu hii yale yasiyokuwemo, basi yatarudishwa kwake.”

Katika upokezi mwingine:

“Mwenye kufanya kitendo ambacho hamna ndani yake dini yetu, atarudishiwa mwenyewe.”[1]

Bi maana hata kama sio yeye aliyeizua.

[1] al-Bukaariy (2697) na Muslim (1718).

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Tafsiyr-ish-Shaykh Muhammad bin ´Abdil-Wahhaab (23) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/tafsirayat-12-07-1435-01_0.mp3
  • Imechapishwa: 20/06/2020