Ni lazima kwa vijana kupambana na matamanio na Hizbiyyah


Enyi vijana wa Kiislamu! Ni lazima tupige vita tamamanio na u-Hizbiyyah. Hizbiyyah ambayo haituletei chochote isipokuwa shari tu na kupotea, udhalilifu na unyonge. Vijana! Tambueni kuwa utukufu kwa aina zake zote na furaha kwa aina zake zote, duniani na Aakhirah, haikudhaminiwa isipokuwa kwa yule mtu ambaye ananyanyua kichwa kwa kufuata yale aliyokuja nayo Muhammad (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na akajitukuza kwayo.

Katika safu za vijana kukipatikana “Allaah amesema” na “Mtume wa Allaah amesema” na vichwa vikanyanyuliwa kwa kusikiliza na kuyatii, basi hapo tutakuwa tumefuata njia sahihi yenye furaha na utukufu duniani na kuokoka na ghadhabu za Allaah na kuingia Peponi na kupata radhi za Allaah (Tabaarak wa Ta´ala). Ama katika safu [za vijana] kukiwa “Fulani na fulani wamesema” na “Pote na pote fulani limesema”, basi tutambue kuwa tunaelekea katika njia ya maangamivu. Naweza kusema kuwa hatuko mwanzoni mwa njia, bali tumeshafika mwisho kabisa wa njia ya maangamivu.

  • Mhusika: ´Allaamah Rabiy´ bin Haadiy al-Madkhaliy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://subulsalam.com/play.php?catsmktba=7539
  • Imechapishwa: 06/09/2020