Swali: Miongoni mwa maovu yaliyodhihiri katika sherehe za harusi ni yale yaliyoenea kwa wanawake wengi katika mavazi yaliyo wazi, yenye kuonyesha na ambayo ni nusu uchi. Je, ni lazima kwa mume kumzuia mke wake kuhudhuria sherehe hii ya ndoa kwa sababu ya maovu haya? Allaah akujaze kheri.
Jibu: Ni lazima kwa mume. Sikilizeni neno ´ni lazima`. Ni lazima kwa mume kumzuia mke wake kuhudhuria sherehe zilizo na maovu. Kwa sababu yeye ni msimamizi juu ya mke wake. Pia ni lazima kwa mke kutekeleza amri ya mume wake. Kwa sababu huu ndio uhakika wa kindoa ambapo anatakiwa kumtii mume katika yasiyokuwa na maana ya kumuasi Allaah. Hali imefikia kiasi cha kwamba wapo baadhi ya wanachuoni waliosema kuwa mume ana ruhusa ya kumzuia mke wake kutoka nyumbani kabisa kabisa. Isipokuwa tu kama anataka kuswali. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msiwazuie wajakazi wa Allaah kutokamana na misikiti ya Allaah.”
Haijuzu kwa mke kukasirika kwa sababu amekatazwa kuhudhuria sherehe hizi za maovu. Bali kinyume chake anatakiwa kumshukuru Allaah kumjaalia mume anayemzuia kutokamana na maasi.
- Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1480
- Imechapishwa: 28/01/2020
Swali: Miongoni mwa maovu yaliyodhihiri katika sherehe za harusi ni yale yaliyoenea kwa wanawake wengi katika mavazi yaliyo wazi, yenye kuonyesha na ambayo ni nusu uchi. Je, ni lazima kwa mume kumzuia mke wake kuhudhuria sherehe hii ya ndoa kwa sababu ya maovu haya? Allaah akujaze kheri.
Jibu: Ni lazima kwa mume. Sikilizeni neno ´ni lazima`. Ni lazima kwa mume kumzuia mke wake kuhudhuria sherehe zilizo na maovu. Kwa sababu yeye ni msimamizi juu ya mke wake. Pia ni lazima kwa mke kutekeleza amri ya mume wake. Kwa sababu huu ndio uhakika wa kindoa ambapo anatakiwa kumtii mume katika yasiyokuwa na maana ya kumuasi Allaah. Hali imefikia kiasi cha kwamba wapo baadhi ya wanachuoni waliosema kuwa mume ana ruhusa ya kumzuia mke wake kutoka nyumbani kabisa kabisa. Isipokuwa tu kama anataka kuswali. Kwani Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Msiwazuie wajakazi wa Allaah kutokamana na misikiti ya Allaah.”
Haijuzu kwa mke kukasirika kwa sababu amekatazwa kuhudhuria sherehe hizi za maovu. Bali kinyume chake anatakiwa kumshukuru Allaah kumjaalia mume anayemzuia kutokamana na maasi.
Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Liqaa´ ash-Shahriy (66) http://binothaimeen.net/content/1480
Imechapishwa: 28/01/2020
https://firqatunnajia.com/ni-lazima-kwa-mume-kumzuia-mkewe-kwenda-katika-sherehe-za-maasi/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)