Ni lazima kwa aliyesilimu kutoa Zakaat-ul-Fitwr?

Swali: Je, Zakaat-ul-Fitwr ni lazima kwa mtu ambaye amesilimu ile siku ya mwisho ya Ramadhaan?

Jibu: Ndio, analazimika kutoa Zakaat-ul-Fitwr kwa sababu hivi sasa ni miongoni mwa waislamu. Ibn ´Umar (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amefaradhisha Zakaat-ul-Fitwr Swaa´ moja ya tende au shayiri kwa wanamme na wanawake, waungwana na watumwa, wadogo na wakubwa kati ya waislamu.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/259)
  • Imechapishwa: 06/05/2021