Swali: Je, inafaa kwa mtu ambaye ni fakiri kuteua mjumbe wa kumpokelea Zakaat-ul-Fitwr kutoka kwa yule anayeitoa katika kipindi chake inapotolewa?

Jibu: Inafaa kufanya hivo. Inafaa kwa yule mwenye kutoa Zakaat-ul-Fitwr kumwambia yule fakiri ateue mtu ambaye atampokelea Zakaat-ul-Fitwr yake wakati inapofika wakati wake. Inapofika wakati wa Zakaat-ul-Fitwr, ambapo ni siku moja au mbili kabla, basi atapewa yule mjumbe ambaye ameteuliwa na yule fakiri.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (18/268-269)
  • Imechapishwa: 06/05/2021