Ni lazima kuwalazimisha watoto kutawadha kabla kugusa Qur-aan?

Swali: Je, ni wajibu kwa mwalimu ambaye anawafunza watoto wadogo Qur-aan kuwalazimisha kutawadha kabla ya kugusa musahafu ikiwa hilo linaweza kupelekea kupoteza sehemu ya muda?

Jibu: Maoni sahihi ni kwamba watoto wadogo mtu anawachukulia usahali kuhusiana na kugusa musahafu:

Mosi: ´Ibaadah si yenye kuwawajibikia.

Pili: Baadhi yao wanaweza kuwa hata hawajui namna ya kutawadha, kama mfano wa wale walio katika shule ya msingi.

Tatu: Huenda sehemu ya muda ikapotea, kama alivosema muulizaji.

Anachopasa ni kuwahimiza kutawadha na awaambie wasije isipokuwa wawe wametawadha. Lakini awafanyie uwepesi fulani. Akitambua kuwa mwanafunzi ameomba idhini ili akatawadhe na kwamba mwanafunzi huyu ni msafi na si mwenye kupenda kutoka klasini, basi impe idhini.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (48) http://binothaimeen.net/content/1094
  • Imechapishwa: 07/04/2019