Swali: Vipi kuhusu ambaye anajizuilia kumuombea du´aa mtawala?
Jibu: Hilo ni katika ujinga wake na kutokuwa na uelewa. Kumuombea du´aa mtawala ni katika mambo makubwa yanayomkurubisha kwa Allaah, utiifu bora na ni katika kutoa nasaha kwa ajili ya Allaah na waja Wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema baada ya kuambiwa kuwa Daws wameasi:
“Ee Allaah! Waongoze Daws na uwalete! Ee Allaah! Waongoze Daws na uwalete!”[1]
Anawaombea watu kheri. Mtawala ana haki zaidi ya kuombewa du´aa, kwa sababu kutengemaa kwake ndio kutengemaa kwa ummah. Kwa hivyo kumuombea du´aa ni katika du´aa muhimu zaidi na ni katika kumtakia mema Allaah amwongoze na kumsaidia katika haki. Aidha amuwafikishe kuwa na matangamano mazuri na amlinde kutokana na shari ya nafsi yake na shari ya wakazi waovu. Kwa hivyo kumuombea du´aa ni katika njia za mafanikio, kutengemaa kwa moyo na matendo yake na pia ni katika mambo muhimu zaidi na ni katika mambo yanayomkurubisha mtu zaidi.
[1] al-Bukhaariy (2779) na Muslim (2524).
- Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Mfasiri: Firqatunnajia.com
- Marejeo: al-Hujj al-Qawiyyah ´alaa Wujuub-id-Difaa´ ´an-id-Dawlah as-Su´uudiyyah, uk. 36
- Imechapishwa: 31/03/2024
Swali: Vipi kuhusu ambaye anajizuilia kumuombea du´aa mtawala?
Jibu: Hilo ni katika ujinga wake na kutokuwa na uelewa. Kumuombea du´aa mtawala ni katika mambo makubwa yanayomkurubisha kwa Allaah, utiifu bora na ni katika kutoa nasaha kwa ajili ya Allaah na waja Wake. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema baada ya kuambiwa kuwa Daws wameasi:
“Ee Allaah! Waongoze Daws na uwalete! Ee Allaah! Waongoze Daws na uwalete!”[1]
Anawaombea watu kheri. Mtawala ana haki zaidi ya kuombewa du´aa, kwa sababu kutengemaa kwake ndio kutengemaa kwa ummah. Kwa hivyo kumuombea du´aa ni katika du´aa muhimu zaidi na ni katika kumtakia mema Allaah amwongoze na kumsaidia katika haki. Aidha amuwafikishe kuwa na matangamano mazuri na amlinde kutokana na shari ya nafsi yake na shari ya wakazi waovu. Kwa hivyo kumuombea du´aa ni katika njia za mafanikio, kutengemaa kwa moyo na matendo yake na pia ni katika mambo muhimu zaidi na ni katika mambo yanayomkurubisha mtu zaidi.
[1] al-Bukhaariy (2779) na Muslim (2524).
Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Mfasiri: Firqatunnajia.com
Marejeo: al-Hujj al-Qawiyyah ´alaa Wujuub-id-Difaa´ ´an-id-Dawlah as-Su´uudiyyah, uk. 36
Imechapishwa: 31/03/2024
https://firqatunnajia.com/ni-kutokana-na-ujinga-wake/
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)