Swali: Ni ipi hukumu ya kwa yule anayenyamaza inapokuja katika suala la Qur-aan imeumbwa au haikuumbwa?

Jibu: Haijuzu. Ni lazima kuamini. Tunaamini kuwa Qur-aan haikuumbwa. Hatusemi kuwa hatujui kuwa imeumbwa au haikuumbwa. Ni kufuru. Ni kama mfano wa mwenye kusema kuwa imeumbwa. Ni mwenye shaka. Ni lazima aazimie na aitakidi kuwa Qur-aan haikuumbwa na kwamba ni Maneno ya Allaah na ni katika sifa Zake. Sifa Zake hazikuumbwa.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Muqaddimati Ibn Abiy Zayd al-Qayrawaaniy fiyl-´Aqiydah (04) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/qir–14331228.mp3
  • Imechapishwa: 17/06/2015