Ni kipindi cha kabla ya Uislamu kwa nisba yake yeye

Swali: Wakati fulani tunamsikia mtu anamwambia mwenzie: “Hiki ni kipindi kabla ya kuja Uislamu (الجاهلية), siku za kughafilika au n.k., akimaanisha kipindi ambapo alikuwa hajanyooka sawasawa..

Jibu: Hapana vibaya. Ni kipindi kabla ya kuja Uislamu kwake yeye. Hapana neno kusema kipindi kabla ya kuja Uislamu na kughafilika muda wa kuwa ni mkweli.

Swali: Lakini kimsemo ni sawa kusema kwamba hiki ni kipindi kabla ya kuja Uislamu?

Jibu: Kipindi kabla ya kuja Uislamu kwake yeye.

Swali: Sio cha aina ile ya kabla ya kuja Uislamu?

Jibu: Kipindi hicho kimeshaondoka. Lakini wale watu ambao wanapuuza Uislamu wako katika kipindi hicho muda wa kuwa wameipa mgongo dini. Wako katika kipindi hicho.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23223/حكم-وصف-الجاهلية-لحال-ما-قبل-الاستقامة
  • Imechapishwa: 29/11/2023