3169- Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Nimemuona Mola wangu katika sura nzuri kabisa. Akasema: ”Ulimwengu wa juu unazozana juu ya kitu gani?” Nikasema: ”Sijui.” Akaweka kiganja Chake cha mkono kati ya mabega yangu mpaka nikahisi ubaridi wa ncha ya vidole Vyake. Kisha Akasema: ”Ulimwengu wa juu unazozana juu ya kitu gani?” Nikasema: ”Juu ya kafara na ngazi.”[1]

Ameipokea at-Twabaraaniy katika ”ad-Du´aa’”.

Kwa kifupi ni kwamba Hadiyth ni Swahiyh. Usahihi wake hautiliwa mashaka na yeyote baada ya kujua njia zake mbalimbali na baadhi ya maimamu kuzisahihisha baadhi yake. Isipokuwa akiwa miongoni mwa wale watu waliojawa na matamanio ambao Allaah amezipofoa nyoyo zao. Mmoja miongoni mwa wapumbavu hao (السخاف) ambaye anaenda kinyume na njia ya waumini na wanachuoni watambuzi. Matokeo yake anayadhoofisha yale waliyosahihisha, ikiwemo Hadiyth hii ambayo ameitungia kijitabu kwa lengo la kuituhumu kwamba imetungwa.

Naapa kwa Allaah kwamba amewasemea uongo. Kwanza imesahihishwa na bingwa wa wenye kuhifadhi ambaye ni Imaam al-Bukhaariy. Vivyo hivyo mwanafunzi wake Imaam at-Tirmidhiy. Ibn ´Abdil-Barr amesema:

“Wanachuoni wamesema kuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona ndotoni. Hadiyth ni nzuri na imepokelewa na waaminifu.”[2]

Mpumbavu (السخاف) huyu anatambua vyema kwamba Hadiyth ambayo wanachuoni wamesema kuwa imetungwa ni ile inayosema:

“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimuona Mola wake ardhini… “

Hii ndio kweli imezuliwa. Hakika mimi nachelea kuna kikosi cha waharibifu kilichoko nyuma ya bwana huyu. Wanamtumia kama kipando kwa ajili ya kuiharibu dini na wanamuwepesishia kutunga na kusambaza ili aweze kuendelea kuwasema vibaya Salaf na wanachuoni, kukusudia kupingana nao na kuwatupia tuhuma za kumfanya mungu kuwa na kiwiliwili (التجسيم). Ya mwisho kutoka kwake ni kwamba ´Aqiydah ya kusema kwamba Allaah yuko juu ya mbingu ni ´Aqiydah ya washirikina na Mushabbihah. Kadhalika jopo la wanachuoni walio wengi ambao wamesahihisha Hadiyth inayosema “Allaah yuko wapi?”, yeye ameidhoofisha; bali amesema kwa kukata kabisa ya kwamab Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kamwe hakusema hivo.

[1] at-Tirmidhiy (3235) amesema:

”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh. Nilimuuliza Muhammad bin Ismaa´iyl juu yake akasema: ”Hadiyth ni nzuri na Swahiyh.”

[2] at-Tamhiyd.

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (7/1/505)
  • Imechapishwa: 23/07/2020