Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:
“Shikamaneni na Sunnah zangu na Sunnah za Makhaliyfah wangu waongofu.”
Naomba nitajia majina makusudio ya “Makhaliyfah waongofu”?
Jibu: Ni wale wane; Abu Bakr, ´Umar, ´Uthmaan na ´Aliy. Hawa ndio Makhaliyfah waongofu.
Imesemekana kuwa ukhaliyfah wa al-Hasan bin ´Aliy ni wenye kukamilisha uongozi wa Makhaliyfah waongofu. Imesemekana vilevile kuwa ´Umar bin ´Abdil-´Aziyz (Rahimahu Allaah) ndiye Khaliyfah wa tano. Lakini lenye kujulikana ni kwamba ni wane. Uongozi wa al-Hasan (Radhiya Allaahu ´anh) ni wenye kukamilisha na hauko kivyake.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (12) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_12.mp3
- Imechapishwa: 15/06/2015
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window)
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window)
- Click to print (Opens in new window)
- Click to email a link to a friend (Opens in new window)
- Click to share on Facebook (Opens in new window)
- Click to share on Twitter (Opens in new window)
- Click to share on Pocket (Opens in new window)