Hakuna dalili ya kubusu msahafu unapomponyoka mtu

Swali: Baadhi ya watu pindi msahafu unapowaponyoka wanaubusu. Ni ipi hukumu ya hilo pamoja na kunitajia dalili?

Jibu: Hakuna dalili ya hilo. Kubusu msahafu ni jambo halina dalili. Msahafu ukimponyoka auchukue na kuupandisha. Hili linatosha kuuheshimisha na himdi ni za Allaah.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh ´Aqiydat-is-Saffaariniyyah (11) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/sfranih_11.mp3
  • Imechapishwa: 01/06/2015