Ni kiasi gani umbali wa kufaa kufupisha swalah?

Swali: Ni kiasi gani umbali wa kufaa kufupisha swalah?

Jibu: Jopo la wanachuoni wengi wanaona kuwa ni mchana mmoja na usiku wake ambapo ni takriban 80 km. Huu ni umbali au masafa kwa njia ya takriban. Wanachuoni wengine wameona kuwa hakuna mpaka wake na kwamba masafa yanatofautiana kutegemea na hali za nchi na hali za wale wasafiri. Lakini hata hivyo kutendea kazi maoni ya jopo la wanachuoni wengi ndio jambo salama zaidi na kuepuka khatari na makosa. Kwa hivyo akisafiri 70 km, 80 km au karibu na hizo basi mtu afupishe swalah. Kama ni karibu na viunga vya mji asifupishe swalah. Hayo khaswa kwa kuzingatia kwamba umbali uliotajwa umepokelewa kutoka kwa Ibn ´Umar na Ibn ´Abbaas ambao ni miongoni mwa wanazuoni wa Maswahabah. Waliweka mpaka yaliyo baina ya Makkah na Twaaif, Makkah na Jeddah. Ndio maana wanachuoni wakasema kuwa ni mchana mmoja na usiku wake.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/4810/%D9%83%D9%85-%D8%A7%D9%84%D9%85%D8%B3%D8%A7%D9%81%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%AA%D9%8A-%D9%8A%D8%AC%D9%88%D8%B2-%D9%85%D8%B9%D9%87%D8%A7-%D9%82%D8%B5%D8%B1-%D8%A7%D9%84%D8%B5%D9%84%D8%A7%D8%A9
  • Imechapishwa: 16/10/2020