Ni ipi tofauti kati ya kufikiwa na dalili na kuifahamu?

Swali: Kuna tofauti kati ya kufikiwa na hoja na kuifahamu?

Jibu: Mwenye kufikiwa na hoja na anaweza kuifahamu na anataka kuifahamu, hoja imemsimamia. Lakini dalili ikimfikia kwa lugha isiyokuwa ya kwake na asiifahamu isipokuwa mpake pale atapotarjumiwa nayo, anapewa udhuru mpaka pale atapobainishiwa maana ya Aayah, Hadiyth au maneno ya wanachuoni kwa lugha yake. Ikiwa iko kwa lugha nyingine awekewe wazi na kutarjumiwa.

Kuhusiana na mwarabu na yule mwenye kufahamu lugha ya kiarabu, hoja imemsimamia pale anapofikiwa na Qur-aan, Sunnah au maneno ya wanachuoni.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Fath-il-Madjîd (25) http://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/fathul%20majid%20-%2027-%2012-%201435.mp3
  • Imechapishwa: 11/02/2017