Ni ipi hukumu ya wanawake kutumia mapesa na mapesa kwa ajili ya saluni?

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuzitengeneza nywele zake kwa njia ya kisasa bila ya kujifananisha na wanawake wa kikafiri?

Jibu: Yaliyotufikia ni kwamba kutengeneza nywele inakuwa ghali. Ni karibu kupoteza pesa. Ninawanasihi wanawake wetu wajiepushe na mtindo huu.

Mwanamke anatakiwa kumpambia mume wake. Lakini sio kwa njia ya kupoteza pesa kama hii. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amekataza kupoteza pesa. Lakini ni sawa endapo ataenda kwa mtengenezaji ambaye atamtengenezea kwa pesa kidogo.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/132)
  • Imechapishwa: 30/06/2017