Ni ipi hukumu ya mwenye kusujudu juu ya paji la uso bila pua?

Swali: Ni ipi hukumu ya mwenye kusujudu juu ya paji la uso bila pua?

Jibu: Sahihi ni kwamba ni lazima kusujudu juu ya pua pia. Haitoshi kusujudu juu ya paji la uso peke yake. Kwa sababu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Nimeamrishwa kujusudu juu ya viungo saba na akaashiria kwa mkono wake pua, mikono miwili, magoti mawili na ncha za vidole.”

Swalah yake inakuwa si sahihi kwa sababu ya kuacha kwake nguzo. Arudi kuswali Rak´ah moja iwapo atakumbuka karibu. Ikiwa kumeshapita muda mrefu basi anatakiwa kuirudi swalah yake yote, ikiwa ni swalah ya faradhi, kama mfano wa nguzo zengine zilizobaki.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: ash-Sharh al-Mumtaaz, uk. 24
  • Imechapishwa: 17/07/2018