74- Jua likishazama, ataondoka kutoka ´Arafah na kuelekea Muzdalifah kwa utulivu na upole. Asisiongamane na watu kwa mwili wake, mnyama wake wa kupanda au gari yake. Atapojipatia nafasi basi akaze mwendo.

75- Atapofika, kuadhiniwe na kukimiwe na kuswaliwe Maghrib Rak´ah tatu. Kisha kukimiwe tena na kuswaliwe ´Ishaa kwa kufupisha na kujumuishwe kati yazo.

76- Atakayetenganisha baina ya swalah hizi mbili kwa sababu ya haja hakuna neno[1].

77- Vivyo hivyo asiswali chochote baina ya swalah hizi mbili wala baada ya swalah ya ´Ishaa[2].

78- Kisha alale mpaka Fajr.

79- Itapombainikia kwamba Fajr imepambazuka, basi aswali mwanzoni mwa kuingia wakati kwa kutoa adhaana na Iqaamah.

[1] Haya ni maoni ya Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah kwa sababu hilo limethibiti kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na Maswahabah wake, kama ilivyotajwa katika “al-Bukhaariy” (25/94/801). Tazama ”Mukhtaswar al-Bukhaariy”.

[2] Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah amesema:

“Atapofika Muzdalifah, basi ikiwezekana aswali Maghrib kabla ya ngamia hajatua magoti chini. Ngamia akishatua magoti yake chini, aswali ´Ishaa. Endapo atachelewesha ´Ishaa, basi hilo halidhuru.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Manaasik-ul-Hajj wal-´Umrah, uk. 30
  • Imechapishwa: 17/07/2018