Ni ipi hukumu ya mwanamke kuswali kwa mkusanyiko?

Swali: Ni ipi hukumu ya mwanamke kuswali kwa mkusanyiko?

Jibu: Hapana neno katika hilo. Anaweza kuswali msikitini nyuma ya imamu. Vilevile wanawake wanaruhusiwa kuswali kwa mkusanyiko ikiwa wamekusanyika pamoja na imamu mwanamke anasimama katikati yao. Imepokelewa kwamba baadhi ya Maswahabiyah wa kike walikuwa wakiswali kwa mkusanyiko. Hata hivyo kuswali kwa mkusanyiko si wajibu juu yao. Kwa hiyo ikiwa wanawake watakusanyika pamoja na wakapenda kuswali kwa mkusanyiko, basi hakuna ubaya katika hilo.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 18/09/2026