Swali: Mtu anayefanya kazi ya mjumbe katika benki inayojihusisha na ribaa. Ni ipi hukumu ya kazi yake na mali yake?

Jibu: Haijuzu kwa mtu kufanya kazi au kushirikiana na benki ya ribaa, wala na yeyote anayejihusisha na ribaa. Allaah (Ta´ala) amesema:

وَتَعَاوَنُوا عَلَى الْبِرِّ وَالتَّقْوَىٰ ۖ وَلَا تَعَاوَنُوا عَلَى الْإِثْمِ وَالْعُدْوَانِ

“Shirikianeni katika wema na uchaji Allaah na wala msishirikiane katika dhambi na uadui.”[1]

Kwa hiyo haifai kwake kuwasaidia kwa jambo lolote wala kuwapa msaada katika shughuli zao.

[1] 05:02

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
  • Imechapishwa: 18/09/2026