Ni ipi hukumu ya kuzika zaidi ya mtu mmoja kwenye kaburi?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuzika zaidi ya mtu mmoja kwenye kaburi moja?

Jibu: Lililowekwa katika Shari´ah ni kila mtu azikwe kwenye kaburi lake. Hivo ndivo ilivyokuwa desturi ya waislamu daima. Lakini kukiwa na haja au dharurah ya kuwakusanya wawili au zaidi kwenye kaburi moja, haina neno. Baada ya vita vya Uhud Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akiwazika watu wawili au watatu kwenye kaburi moja. Katika hali hii inatakiwa kumtanguliza karibu na Ka´bah yule ambaye ni mjuzi wao zaidi wa Qur-aan, kwa kuwa yeye ndiye mbora wao. Wanatakiwa kulazwa kwa kukaribiana. Wanachuoni wanasema inatakiwa kuweka kizuizi cha udongo baina yao.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/214)
  • Imechapishwa: 25/08/2021