Ni ipi hukumu ya kuwaunga ndugu?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuwaunga ndugu?

Jibu: Ni jambo la lazima. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

”Yule anayependa akunjuliwe riziki yake na arufushiwe maisha yake basi aunge kizazi chake.”

Amesema katika Hadiyth Swahiyh nyingine kuhusu kuunga kizazi:

”Yule atakayekiunga, basi nami nitamuunga, na yule atakayekikata, basi nami nitamkata”

Allaah (Ta´ala) amesema:

فَهَلْ عَسَيْتُمْ إِن تَوَلَّيْتُمْ أَن تُفْسِدُوا فِي الْأَرْضِ وَتُقَطِّعُوا أَرْحَامَكُمْ أُولَـٰئِكَ الَّذِينَ لَعَنَهُمُ اللَّـهُ فَأَصَمَّهُمْ وَأَعْمَىٰ أَبْصَارَهُمْ

”Basi huenda nyinyi mkigeuka ndio mfanye ufisadi katika ardhi na kukata jamaa zenu wa uhusiano wa damu? – hao ndio wamewalaani na Allaah akawafanya viziwi na akawapofua macho yao.”[1]

 Katika Hadiyth nyingine imekuja:

”Hatoingia Peponi yule mwenye kukata kizazi.”

[1] 47:22-23

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaad-ud-Duruus https://binbaz.org.sa/fatwas/6831/%D9%85%D8%A7-%D8%AD%D9%83%D9%85-%D8%B5%D9%84%D8%A9-%D8%A7%D9%84%D8%B1%D8%AD%D9%85
  • Imechapishwa: 08/01/2021