Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali Witr? Ni jambo maalum katika Ramadhaan peke yake?

Jibu: Sunnah ni Sunnah iliyokokotezwa katika Ramadhaan na miezi mingine. Imaam Ahmad amefikia mpaka kusema kwamba yule mwenye kuacha kuswali Witr ni mtu muovu na haitakiwi kuukubali ushahidi wake. Kwa hiyo ni Sunnah iliyokokotezwa na muislamu hatakiwi kuiacha sawa katika Ramadhaan na miezi mingine.

Witr ni kule kuimaliza swalah ya usiku kwa Rak´ah moja. Witr sio kama wanavyofahamu baadhi ya wale wasiokuwa na elimu kwamba ni ile Qunuut. Qunuut ni kitu kimoja na Witr ni kitu kingine. Witr ni kule kuimaliza swalah ya usiku kwa Rak´ah moja au kwa Rak´ah tatu kwa mpigo. Kwa hali yoyote Witr ni Sunnah iliyokokotezwa sawa katika Ramadhaan na miezi mingine. Muislamu hatakiwi kuiacha.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/114)
  • Imechapishwa: 17/06/2017