Kusimama usiku na kuswali au kujifunza elimu usiku?

Swali: Ni ipi bora zaidi kati ya kusimama usiku na kuswali na kutafuta elimu?

Jibu: Kujifunza elimu ndio bora kuliko kusimama usiku na kuswali. Kujifunza elimu, ni kama alivyosema Imam Ahmad, hakulinganishwi na kitu midhali mtu nia yake ni njema. Anatakiwa kunuia kujiondoshea ujinga kwanza yeye na wengine.

Ikiwa mtu anaamka usiku kwa ajili ya kujifunza elimu kwa ajili ya Allaah pekee, ni mamoja akawa ni mwanafunzi anayesomeshwa au akawa ni mwalimu anayesomesha watu, hilo ni bora kuliko kusimama usiku na kuswali. Akiweza kuyafanya yote mawili ndio bora zaidi na zaidi. Lakini yakishindikana yote mawili basi kujifunza elimu ndio bora na ndio lenye haki zaidi. Kwa ajili hii ndio maana Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwamrisha Abu Hurayrah aswali Witr kabla ya kulala. Wanachuoni wamesema kuwa sababu ya hilo ni kuwa Abu Hurayrah alikuwa akizihifadhi Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mwanzoni mwa usiku na akilala mwishoni mwa usiku. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwelekeza kuswali Witr kabla ya kulala.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (14/113)
  • Imechapishwa: 17/06/2017