Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya nguo yenye kuonyesha ndani?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya nguo yenye kuonyesha ndani?

Jibu: Inatokea wakati wa majira ya joto baadhi ya watu wanaswali ndani ya nguo nyepesi. Kwa ndani wanakuwa na kaptula isiyofika magotoni. Kitendo hicho ni haramu. Haijuzu kuswali na nguo kama hizo. Moja katika sharti za swalah ni mtu afunike kile kilicho baina ya kitovu na magoti yake. Kaptula haifuniki kile kilicho baina ya kitovu na magoti yake. Nguo nyepesi inaonyesha rangi ya ngozi kwa ndani yake. Kwa maana nyingine anakuwa hakufunika ile sehemu ya siri ambayo analazimika kuifunika. Katika hali hiyo vyovyote atakavyoswali swalah yake inakuwa batili. Kwa ajili hiyo ni lazima kwa ndugu zetu wavae suruwali inayofunika kati ya kivotu na magoti au wavae nguo nene isiyoonyesha kwa ndani.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/263-264)
  • Imechapishwa: 19/03/2026