Ni ipi hukumu ya kusoma “Yaa Siyn” baada ya kuzika?

Swali: Ni ipi hukumu ya kusoma “Yaa Siyn” baada ya kumzika maiti?

Jibu: Kusoma “Yaa Siyn” kwenye makaburi ni Bid´ah na halina asli. Sio Sunnah kusoma Qur-aan baada ya kuzika. Ni Bid´ah. Pindi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alipokuwa anamaliza kuzika anasimama karibu na kaburi na kusema:

“Muombeeni msamaha ndugu yenu na mumtakie uthabiti. Hakika hivi sasa ataulizwa.”[1]

Hakuna dalili yoyote ya kwamba (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akisoma Qur-aan kwenye makaburi wala hakuliamrisha.

[1] Abu Daawuud (3221).

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/222)
  • Imechapishwa: 02/09/2021