Ni ipi hukumu ya kupaweka mataa makaburini?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuweka mataa makaburini?

Jibu: Makaburi ambayo watu hawahitajii, kama kwa mfano sehemu ya makaburi kukawa ni papana ambapo wameshamaliza sehemu yote kuwazika watu, hakuna haya ya kuweka mataa.

Ama sehemu ambapo bado kuna nafasi kukaangazwa pembezoni mwake inaweza kusemwa kuwa inafaa. Hakutaangazwa isipokuwa usiku tu. Katika hilo hakuna chochote kinachoonyesha kuwa makaburi yanaadhimishwa. Katika hali hii yatatumiwa wakati wa haja. Lakini mimi naonelea kuwa ikatazwe kupaangaza kabisa kutokana na sababu zifuatazo:

1- Hakuna udharurah.

2- Kukiwa kuna dharurah, watu walete mataa yao.

3- Jambo hili likifunguliwa basi kuna khatari likapea na matokeo yake ikasindikana kulidhibiti.

Ama ikiwa makaburini kuna chumba ambacho kunawekwa ndani yake kokoto na vinginevyo, haina neno kukiweka mataa kwa kuwa kiko mbali na makaburi. Mataa yako kwa ndani na hayaonekani.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (17/208-209)
  • Imechapishwa: 25/08/2021